Wametufunga lakini ‘shughuli’ wameiona

Pamoja na kupoteza mchezo wa leo kwa bao moja dhidi ya Al Ahly, wachezaji wetu wamepambana muda wote na kuonyesha upinzani mkubwa.

Mchezo huo ulikuwa wa mwisho kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Haikuwa tofauti kubwa ndani ya uwanja huku kukiwa na uwiano ambao ulikuwa burudani kwa watazamaji kutokana na ubora wa wachezaji wa timu zote.

Ahly walipata bao la kwanza dakika ya 31 kupitia kwa Mohammed Elshanawy kufuatia mpira wa krosi kutoka upande wa kushoto kuokolewa na mlinda mlango Aishi Manula kabla ya kumkuta mfungaji akiwa yupo chini.

Baada ya bao hilo timu zote zilishambuliana kwa zamu huku kasi ya mchezo ikiongezeka kadri muda ulivyozidi kusonga.

Dakika 10 za mwisho tuliongeza kasi kwa kuliandama zaidi la Ahly ambao muda wote walikuwa nyuma na kutengeneza mashambulizi makali ambayo hata hivyo hayakuweza kubadili matokeo.

Kocha Didier Gomez aliwaingiza Francis Kahata, Mzamiru Yassin, Chris Mugalu na Hassan Dilunga kuchukua nafasi za Rally Bwalya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni na Mohammed Hussein.

Droo ya hatua ya robo na nusu fainali itapangwa Aprili 30 ambapo tutapangwa na timu iliyomaliza nafasi ya pili baada ya sisi kumaliza vinara.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER