Waliokuwa Stars wajiunga na wenzao mazoezini

Nyota wanne ambao walisafiri na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kuelekea Algeria leo wamejiunga na wenzao na kufanya mazoezi jioni.

Nyota hao ni washambuliaji nahodha John Bocco na Kibu Denis kiungo, Mzamiru Yassin na mlinzi, Kennedy Juma.

Kikosi chetu leo kimerejea mazoezini kufuatia mapumziko ya siku moja baada ya mchezo wa kirafiki tuliocheza Jumamosi dhidi ya Ngome na kuibuka na ushindi wa mabao 6-0.

Tunaendelea na maandalizi ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos utakaopigwa Septemba, 16 katika Uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola; Zambia.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER