Wachezaji wote ni muhimu Simba

Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe, ameweka wazi kuwa kila mchezaji ana umuhimu sawa ndani ya kikosi na lengo lake ni kuhakikisha timu inapata ushindi kila anapokuwa uwanjani.

Kapombe amesema Simba imefanya usajili wa wachezaji 30 kwa ajili ya msimu huu na kila mmoja ana umuhimu sawa ndiyo maana kocha amekuwa akifanya mabadiliko ya kikosi mara kwa mara.

Katika mchezo wa leo wa Azam Sports Federation Cup dhidi ya JKT Tanzania kocha Pablo Franco amewatumia wachezaji wengi ambao hawajapata nafasi katika mechi zetu zilizopita na wamefanya vizuri.

“Kila mchezaji ana umuhimu sawa ndani ya kikosi chetu, tumesajili wachezaji 30 kwa ajili ya msimu huu na kila anayepata nafasi yupo tayari kuipigania timu. Kocha ndiye anaamua amtumie nani katika mechi husika,” amesema Kapombe.

Akizungumzia mchezo dhidi ya maafande hao Kapombe amesema ulikuwa mgumu kutokana JKT kushuka daraja na hatujakutana kwa muda mrefu kwa hiyo tulitumia muda mrefu kuwasoma kipindi cha kwanza.

“Ukiangalia kipindi cha kwanza mchezo ulikuwa mgumu ingawa tulipata bao la mapema lakini cha pili tulikuwa bora tukatengeneza nafasi lakini hatukuwa na bahati,” amesema Kapombe.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER