Wachezaji wasiojituma watapigwa ‘Thank You’

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ ameweka wazi kuwa wachezaji ambao hawataonyesha uwezo wao na kujituma uwanjani hawatuvumiliwa hivyo wataachwa.

Try Again amesema katika kipindi cha mwezi mmoja na siku chache kilichobaki kuelekea dirisha dogo la usajili kila mchezaji anapaswa kujituma na kuonyesha uwezo wake la sivyo ataachwa.

Try Again ameongeza kuwa Simba haiwezi kuwa na wachezaji ambao wanalipwa kiasi kikubwa cha pesa na bado wanakaa benchi kutokana viwango kushuka.

“Baada ya matokeo tuliyopata siku za karibuni tumefanya tathimini ili kuona tumekwa wapi na tumegundua wachezaji wengi hawajitumi. Tumewaambia hatuta wavumilia kila mmoja anapaswa kujituma,” amesema Try Again.

Akizungumzia dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa mwezi ujao Try Again amesema “tutasajili lakini kwa mapendekezo ya mwalimu mpya ambaye tutamtangaza karibuni.

“Unajua unaweza kumsajili mchezaji hata kutoka Al Ahly lakini akaja hapa na kocha asimtumie, tutampa jukumu hilo yeye kwakuwa ndiye anajua anataka mchezaji wa aina gani kwenye kikosi chake,” amesema Try Again.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER