Wachezaji wetu pamoja benchi la ufundi leo wamepimwa Covid-19 tayari kwa maandalizi ya safari ya kuelekea Botswana itakayokuwa Ijumaa jioni.
Kupima Covid-19 kabla ya safari kutoka nchi moja hadi nyingine ni utaratibu uliowekwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo.
Kikosi kinaelekea Botswana tayari kwa mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galax utakaopigwa Jumapili, Oktoba 17.
Tayari wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya timu za taifa wameanza kurejea huku wale waliokuwa Taifa Stars wakifanya mazoezi na wenzao leo.