Wachezaji wapewa mapumziko kesho kuanza kuivutia kasi Tanzania Prisons

Baada ya timu kurejea kutoka nchini Sudan wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja ambapo kesho wataanza mazoezi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Jumatano Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kikosi kimetua nchini mchana wa leo na wachezaji wamepewa muda wa kwenda kuonana na familia zao na kesho wataanza mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Prisons.

Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu amesema kikosi kitaanza mazoezi kesho jioni kwenye viwanja vyetu vya Mo Simba Arena na wachezaji wote watahudhuria.

“Wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja baada ya kurejea kutoka Sudan na kesho jioni wataanza mazoezi kujiandaa na mchezo wa Ligi dhidi ya Tanzania Prisons,” amesema Rweyemamu.

Tutaingia kwenye mchezo wa Jumatano tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 tulioupata kwenye mechi ya ligi iliyopita dhidi ya JKT Tanzania.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER