Wachezaji wapewa mafunzo ya awali

Wachezaji wetu leo wamepewa mafunzo ya awali (Orientation) ya kitu gani wanatakiwa kukifanya kabla kuanza maandalizi ya msimu na baadae mashindano yenyewe.

Mafunzo hayo yameongozwa na Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula ambayo yaliambatana na utambulisho kwa wachezaji.

Kajula amewaelekeza wachezaji dhamira ya Uongozi, Wanachama pamoja na mashabiki wanachohitaji kuelekea kuanza kwa msimu wa mashindano 2024/25.

Wachezaji wapya wamepatana nafasi ya kukutana na wenzao na kubadilishana mawazo na wapo tayari kwa maandalizi ya msimu.

Mafunzo hayo pia yamehudhuriwa na benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Fadlu Davids.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER