Wachezaji wamepata maandalizi mazuri kuelekea Derby ya Kariakoo Kesho

Mlinzi wa kulia ambaye ni mchezaji mwandamizi ndani ya kikosi chetu, Shomari Kapombe amesema wamepata maandalizi mazuri kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga.

Kapombe amesema wiki moja waliopata ya kujiandaa na mchezo huo mkubwa Afrika yametosha na anaamini tutafanikiwa kupata ushindi.

Mlinzi huyo ambaye ni miongoni mwa wachezaji waliocheza mechi nyingi za Derby amesema inapofika siku kama ya kesho huwa hana presha na anajitahidi kufanya vizuri ili kuisaidia timu kupata ushindi.

Kapombe amesema wachezaji wanafahamu mchezo huo umebeba hisia za mashabiki hivyo watahakikisha wanapambana ili kuwapa furaha.

“Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari, tumepata wiki moja ya maandalizi ambayo inatufanya tuwe tayari kwa mchezo wa kesho.

“Tunafahamu mchezo wa kesho una presha kubwa na unabeba hisia kwa mashabiki na huwa unatazamwa sana sisi wachezaji tumejiandaa kwa kila kitu kuhakikisha tunashinda na kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Kapombe.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER