Wachezaji wafanyiwa vipimo kabla ya kupaa Misri

Wachezaji wetu wamefanyiwa vipimo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo, kabla ya kusafiri kuelekea nchini Misri tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi (Pre Season) kesho.

Daktari wa timu Edwin Kagabo, amesema wachezaji wamepimwa magonjwa mbalimbali yakiwemo ya moyo ili kuhakikisha wanaanza msimu wakiwa fiti.

Timu nyingi duniani zimeweka utaratibu wa kuwafanyia vipimo  wachezaji kabla ya kuanza msimu mpya ili kuhakikisha usalama wao baada ya kutoka mapumzikoni.

“Huu ni utaratibu ambao upo duniani kote leo wachezaji wetu wamefanyiwa vipimo vya afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kujua utimamu wao kabla ya kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi,” amesema Dk. Edwin.

Baada ya vipimo hivyo kikosi kitaondoka kesho mchana kuelekea Misri tayari kuanza maandalizi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER