Wachezaji wetu wamepewa siku tatu za mapumziko kutokana na kusimama kwa ligi kupisha mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia
Wachezaji ambao hawajaitwa katika timu zao za taifa watarejea mazoezini baada ya muda huo huku wale walioitwa wakiruhusiwa kwenda kujiunga kwenye nchi zao.
Nyota wetu tisa watajiunga na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayojiandaa na mechi mbili za kufuzu dhidi ya DR Congo na Madagascar huku wale wakigeni nao wakitarajia kuondoka.
Mchezo wetu wa kwanza baada ya ligi kurejea utakuwa dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Novemba 19, Uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza.
One Response