Wachezaji Simba wafanyiwa vipimo vya moyo

Nyota wetu wote 32 tuliowasajili kwa ajili ya msimu mpya wa ligi 2021/22 leo mchana wamefanyiwa vipimo vya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Wachezaji wamepimwa vipimo vyote vinavyohusu moyo ukiwemo mfumo wa umeme unavyofanya kazi ndani ya mwili.

Haya ni maelekezo ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kuwa wachezaji wanapaswa kufanyiwa vipimo hivyo kabla ya kuanza msimu wa mashindano.

Kumekuwa na matukio mengi duniani ya wachezaji kuanguka uwanjani kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi ambayo wakati mwingine husababisha vifo ndiyo maana CAF wanasisitiza wachezaji kufanyiwa vipimo hivyo.

Kikosi chetu kitaanza mikiki mikiki ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza kwa kucheza na Jwaneng Galaxy kutoka Botswana kati ya Oktoba 15 na 16 ugenini na marudiano yatakuwa kati ya Oktoba 22 na 23 hapa nchi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER