Viongozi wakutana na wachezaji kabla ya kuivaa Vipers

Saa chache kabla ya kushuka katika uwanja wa St. Mary’s kuikabili Vipers katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Viongozi wa klabu wamekutana na wachezaji kuwakumbusha umuhimu wa kupata alama tatu leo.

Viongozi hao wameongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mungungu, Wenyeviti wazamani Ismail Aden Rage na Swedi Mkwabi.

Wengine ni Katibu Mkuu wazamani, Hassan Hassanoo Mjumbe wa Bodi wazamani Hassan Kipusi pamoja Mjumbe wa Bodi ya sasa CPA Issa Masoud.

Akizungumzia kwa niaba ya viongozi hao, Mwenyekiti wa Bodi, Try Again amewasisitiza wachezaji kuhakikisha wanapambana kuanzia dakika ya kwanza mpaka mwisho ili ushindi unapatikane kwakuwa furaha ya Wanasimba ipo mabegani mwao.

“Binafsi nawaamini sana nyinyi, mnaweza kushinda mchezo wa leo. Kikubwa hakikisheni mnatumia vizuri nafasi na kuongeza umakini. Najua mnaweza kuwafanya Wanasimba wakafurahi leo,” amesema Try Again.

Kwa niaba ya wachezaji, nahodha John Bocco amesema wanajua umuhimu wa mchezo wa leo na yoyote atakayepewa nafasi ya kucheza atakuwa tayari kuipigania timu.

“Hata bila ya kuambiwa sisi wenyewe wachezaji tunajua tunatakiwa kushinda mchezo wa leo, tunahitaji kuvuka hatua hii, tutapambana mpaka dakika ya mwisho ili tupate ushindi,” amesema Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER