Viingilio vya mchezo wetu dhidi ya Mbeya City

Viingilio vya mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City tayari vimetangazwa ambapo kiingilio cha chini itakuwa Sh 5,000.

Mchezo huo wa ligi ambao ni wa kwanza tangu kuanza kwa mwaka 2023, utapigwa Jumatano saa moja usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo huo utakuwa ni wa kwanza kwa Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ambaye atarejea kesho pamoja na kikosi kutoka Dubai tulipoweka kambi ya siku nane.

Mchezo huo pia tutautumia kuwatambulisha wachezaji wetu wapya tuliowasajili katika dirisha la usajili ambalo limefungwa jana.

Viingilio vipo kama ifuatavyo:

Mzunguko Sh 5,000
VIP B na C Sh 10,000
VIP A Sh 15,000

Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kupitia mitandao ya simu na vituo pia vimetangazwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER