Viingilio Ngao ya Jamii vyatangazwa

 

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ngao ya Jamii kati yetu na watani wetu wa jadi Yanga.

Mchezo huo ambao utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa utaanza saa moja usiku badala ya saa 11 jioni kama ilivyozoeleka.

Mchezo huo ni wa kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya NBC 2022/23 ambayo itaanza rasmi Agosti 17.

Viingilio hivyo ni kama ifuatavyo;

VIP A Sh. 30,000
VIP B Sh. 20,000
VIP C Sh. 15,000
Viti vya machungwa Sh. 7,000
Viti vya kijani Sh. 5,000

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER