Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu Ahmed Ally amesema katika mchezo wa jana dhidi ya Al Ahli Tripoli wachezaji walitimiza majukumu yao kwa asilimia 100 na kutupa matokeo mazuri ugenini.
Ahmed amesema baada ya wachezaji kufanya hivyo mechi inayofuata ni ya mashabiki kutimiza majukumu yao kwa asilimia 100 na kujitokeza kwa wingi uwanjani kama walivyofanya wapinzani wetu jana ili kuongeza hamasa.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Ahmed amezungumzia pia kuhusu ratiba ya timu kurejea nchini.