Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu Ahmed Ally amesema kikosi chetu kitaondoka kesho kuelekea Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi ya siku saba kujiandaa na mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Machi 29.
Ahmed amesema kambi hiyo ya Zanzibar itahusisha wachezaji ambao hawakuitwa kwenye timu zao Taifa ambao ni wengi ili kumpa nafasi kocha kufanya maandalizi ya kutosha kutokana na ukubwa wa mechi.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Ahmed ataja sababu ya timu kwenda kuweka kambi Zanzibar.