Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa amekabidhi kitita cha milioni 10 kwa wachezaji ikiwa ni zawadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Saluhu Hassan baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya CS Constantine kutoka Algeria.
Mh. Msigwa amesema Rais Samia anawapongeza wachezaji kwa kazi kubwa waliyofanya ya kuibuka na ushindi huo muhimu katika mchezo ambao haukuwa na mashabiki.
Tazama video hii hadi mwisho kiungo mkabaji Fabrice Ngoma ameahidi ushindi mnono zaidi katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Al Masry utakaopigwa mwezi Aprili.