Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema licha ya ushindi wa mabao 2-0 tuliopata dhidi ya APR kwenye kilele cha Simba Day lakini bado miili ya wachezaji wetu haijafunguka.
Fadlu amesema tumekuwa na wiki tatu za maandalizi ngumu kule Misri na tumerejea tumekutana na mechi ngumu ndio maana miguu ya wachezaji imekuwa migumu hasa kipindi cha kwanza.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Kocha Fadlu amezungumzia pia mchezo unaofuata wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii.