Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema vibali vya wachezaji wote vitakuwa vimepatikana kabla ya kuanza mchezo wetu wa kesho dhidi ya Singida Fountain Gate FC.
Ahmed amesema utaratibu wote umefanyika ilikuwa imebaki malipo ambapo kila kitu kitakaa sawa kabla ya mchezo wa kesho.
Tazama hadi mwisho mahojiano haya ili kujua maandalizi ya timu yalivyo mpaka sasa.