‘Vibe’ la Wanasimba Kigamboni usipime

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amewaongoza mashabiki na wapenzi wa Simba Kigamboni kuhamasisha kuelekea mchezo wetu wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja Usiku.

Shamra shamra zilianzia kwenye kivuko cha Pantoni mpaka Kigamboni na kurudi katika Soko la Samaki Feri ambapo vikundi mbalimbali vya ngoma vilikuwa vikitumbuiza mwanzo mwisho.

Ahmed amewasisitiza mashabiki kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi uwanjani baada ya kuruhusiwa kuujaza na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Ahmed ameongeza kuwa mchezo wa Jumapili ni muhimu sana kwetu kupata ushindi mnono kwa sababu tumedhamiria kutinga nusu fainali ya michuano hiyo, hivyo ni vizuri tukamaliza kazi nyumbani.

“Wanasimba wenzangu Jumapili hakuna kazi nyingine zaidi ya kujitokeza uwanjani kuipa sapoti timu ili kufanisha lengo la kutinga nusu fainali. Wakina Kapombe, Kagere, Bwalya peke yao hawatoshi bila sapoti yenu,” amesema Ahmed.

Zoezi hili la kuhamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani Jumapili limeingia siku ya pili baada ya kuzinduliwa jana na Mwenyekiti wa klabu upande wa wanachama, Murtaza Mangungu Temeke Maduka Mawili jijini Dar es Salaam.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER