‘Vibe’ la Simba Chalinze Usipime

Mamia ya mashabiki wamejitokeza kwa wingi mjini Chalinze kwa ajili ya hamasa kuelekea mchezo wetu wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa Jumamosi, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ukiacha magari yalitoka jijini Dar es Salaam na mashabiki pamoja na Waandishi wa Habari pia njiani tumekutana na Matawi mengine ya Simba ambayo tulijiunga nao hadi Chalinze.

Tulivyofika Chalinze tumepokelewa na msafara wa Bodaboda ambao tulizunguka nao maeneo mbalimbali ya Chalinze mjini.

Balaa zito limefanyika ‘Round About’ ya Chalinze ambapo magari, Bodaboda pamoja na mashabiki waliokuwa wanatembea kwa miguu walikuwa wakishangilia wakiongozwa na watu wa hamasa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER