Valentino Mashaka ni Mnyama

Tumeinasa saini ya mshambuliaji kijana, Valentino Mashaka kutoka Geita Gold kwa mkataba wa miaka miwili.

Valentino mwenye umri wa miaka 18 ni kijana mwenye kipaji na uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza nafasi hivyo tumemuona kama mtu sahihi katika ujenzi wa kikosi chetu kipya.

Msimu uliopita Valentino amehusika katika mabao saba, akifunga sita na kusaidia kupatikana kwa jingine moja (assist).

Ikiwa inathibitisha uwezo aliouonyesha msimu uliopita ameshinda mara mbili mchezaji bora wa mwezi wa klabu kwa tuzo zilizokuwa zinatolewa kwa wachezaji wa Geita Gold.

Valentino ni kijana Mtanzania mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kutumia nafasi na hicho ni moja ya kitu kilichotuvutia kupata saini yake.

Uongozi wa klabu unaendelea kusajili wachezaji bora katika kila nafasi ili ikitokea mmoja akikosekana kwa sababu yoyote kusiwe na pengo.

Valentino Mashaka anaungana na Washambuliaji wengine Steven Mukwala na Freddy Michael na kufanya Simba kuwa na idadi ya Washambuliaji watatu bora

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER