Ushindi wa Dodoma umetuongezea morali kuelekea Shirikisho Afrika

Kocha Mkuu Pablo Franco amesema ushindi wa mabao 2-0 tuliopata dhidi ya Dodoma Jiji utaongeza morali kwa wachezaji kuelekea maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane.

Baada ya mchezo wa Dodoma hatutakuwa na mechi nyingine hadi Machi 13 tutakapokutana na Berkane katika mtanange utakaopigwa Uwanja wa Taifa.

Akiuzungumzia mchezo dhidi ya Dodoma, Pablo amesema tulicheza vizuri tulitengeneza nafasi nyingi na kutawala sehemu kubwa lakini kipindi cha kwanza hatukuweza kuzitumia.

“Tulitawala sehemu kubwa ya mchezo tulitengeneza nafasi nyingi hasa kipindi cha kwanza. Jambo zuri kuna wachezaji walikuwa majeruhi muda mrefu tumewapa nafasi dakika chache ili kuwarejesha katika hali za kawaida.

“Ushindi huu umeongeza morali kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Berkane. Tutafanya maandalizi mazuri kabla ya mchezo huo ambao ni muhimu sana kwetu,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER