Kiungo mshambuliaji, Rally Bwalya amesema alishangilia kwa staili ya ishara ya kuonyesha saa ya mkononi akimaanisha imefika hatua ya kupata mafanikio kuanzia kwenye Ligi za ndani hadi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Bwalya alifunga bao hilo ambalo lilikuwa la pili kwenye ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa dakika ya 19 baada ya kupokea pasi ya Shomari Kapombe akiwa ndani ya kisanduku na kumpiga chenga mlinzi mmoja na kuweka mpira kambani.
“Nilishangilia kwa staili ya kupiga mkononi sababu nilikuwa naonyesha muda wa Simba kufanya vizuri ndani na nje ya nchi umefika,” amesema Bwalya.
Raia huyo wa Zambia amesema kwa sasa tupo kwenye kiwango bora na muda wetu wa kufanya vizuri kwenye ligi zote umefika.
Bwalya ameongeza kuwa amefurahi kufunga bao lake la kwanza kwenye Ligi Kuu sababu ndiyo lengo la kila mchezaji kuisaidia timu.
“Simba ni timu kubwa na ipo kwenye kiwango bora sasa ni wakati wa kila mchezaji kuisaidia ili kupiga hatua kwenda mbele zaidi,” amesema Bwalya.
3 Responses
🦁🦁🦁
Kabisaaaaaaaa hii inafaida sana kwa timu yetu pendwa y Simba