Ujenzi ukuta Bunju wafikia asilimia 70

Kamati ya Maendeleo ya Bunju imetembelea ujenzi wa ukuta wa uzio wa uwanja wetu wa Mo Simba Arena uliopo Bunju ambapo hadi sasa umefikia asilimia 70.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Crescentius Magori amesema hadi wa mwezi huu uzio huo utakuwa umekamilika na hatua ya kwanza itakuwa tayari.

Magori amesema baada ya kukamilika kwa hatua ya kwanza kamati itakaa chini kufanya upembuzi yakinifu na kuangalia hatua ya pili ya ujenzi ambayo itakuwa ni hosteli za timu zote tatu, gym mabwawa ya kuogelea na kila kitu ambacho kinahitajika kwa timu.

“Ujenzi umefikia asilimia 70 hadi sasa, tunategemea ikifika mwisho wa mwezi huu utakuwa umekamilika na tutakaa tena kuangalia kitu gani kitafuata baada ya hatua hii,” amesema Magori.

Mkandarasi wa ujenzi huo, Jonathan Kibona amesema vifaa wanavyotumia kwenye ujenzi huo ni imara na vya kisasa ili kudumu kwa muda mrefu.

“Kama mlivyoona ujenzi unaendelea vizuri na tuliahidi mpaka ikifika mwisho wa mwezi huu tutakuwa tumekamilisha hatua ya kwanza ya ujenzi. Tunatumia vifaa vya kisasa ili kulifanya liwe imara,” amesema Kibona.

Mwenyekiti wa klabu upande wa Wanachama, Murtaza Mangungu amesema fedha zote zilizochangwa na wanachama kupitia ‘Nani Zaidi’ pamoja na zile zilizotolewa na Rais wa Heshima, Mohamed Dewji ‘Mo’ zitatumika kama zilivyokusudiwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER