Kikosi chetu cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kimetinga nusu fainali ya baada ya kuifunga JKT Tanzania bao moja katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Mchezo ulianza kwa kasi huku JKT wakitushambulia kwa kasi huku mlinda mlango wetu Ahmed Feruzi akifanya kazi kubwa ya kuokoa michomo.
Goli pekee kwenye mchezo huo lililofungwa na Samson Lucas lilifungwa kwa shuti kali lililomponyoka mlinda mlango wa JKT, Mohamed Bomoa dakika ya 66.
Kocha Nico Kiondo aliwatoa Athumani Abdul, Baraka Shaban na Godfrey George na kuwaingiza Andrew Michael, Kasim Omary na Omary Abdallah.
Tumemaliza hatua ya makundi tukiwa na alama saba sawa na vinara tukimaliza nafasi ya pili kwenye msimamo tukizidiwa mabao ya kufunga.
Mchezo wa wetu wa nusu fainali utapigwa Juni 17 na atakayemaliza kinara wa kundi B katika dimba hilo hilo la Azam Complex.