U20 yashindwa kutinga Fainali Michuano ya TFF

Timu yetu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 imeshindwa kutinga fainali ya michuano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupoteza kwa bao moja dhidi ya Azam katika mchezo wa Nusu Fainali uliopigwa Uwanja wa JK Youth Park.

Mchezo huo ulianza kwa kasi timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini zikikosa ubunifu katika eneo la mwisho.

Dakika ya 32 Azam walipata bao pekee kupitia Jamal Ozil baada ya beki wetu wa kati kufanya makosa.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi ya mashambulizi na kutengeneza nafasi lakini Azam walikuwa wote nyuma wakizuia.

Hata hivyo vijana hao wa Mussa Mgosi walikosa bahati maana dakika 10 za mwisho walifanya mashambulizi mengi langoni mwa Azam lakini halikupatikana bao.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER