Tutakutana na mshindi kati ya Uhamiaji na Libya 1 Kombe la Shirikisho Afrika

Droo ya Kombe la Shirikisho Afrika imekamilika na tutakutana mshindi kati ya Uhamiaji FC ya Zanzibar au Libya 1 katika hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Simba ni miongoni mwa timu ambazo hazitaanzia hatua ya awali bali itasubiri hadi hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mshindi kati ya Uhamiaji na Libya 1 tutakutana nae katika mchezo wa hatua ya kwanza kati ya Septemba 13-15 na marudio yatakuwa kati ya Septemba 20-22.

Katika mchezo huo tutaanzia ugenini kwenye mechi ya mkondo wa kwanza na marudiano tutakuwa nyumbani.

Mshindi wa jumla katika mchezo wa hatua ya kwanza atafanikiwa kupata tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER