Tutacheza na Power Dynamo Simba Day

Kama ilivyo ada kwenye kilele cha Simba Day ambacho kimedhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya sherehe na shamra shamra za utambulisho wa wachezaji huwa inakamilika kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa.

Safari hii kilele cha Simba Day kitakuwa Agosti 6 na tutacheza na Power Dynamo ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Zambia.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema tumewachagua Power Dynamo kwakuwa ni timu bora na ndio itaiwakilisha Zambia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na wao ndio mabingwa wa nchi.

“Power Dynamo ndio timu ambayo tutacheza nayo kwenye kilele cha Simba Day Agosti 6 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa,” amesema Ahmed Ally.

Kama ilivyo kawaida kabla ya kilele kunakuwa na matukio mbalimbali ya kutoa kwa jamii kama kutoa damu, kutembelea wagonjwa Hospitali, kufanya usafi maeneo mbalimbali.

Zoezi la kuchangia damu litakuwa ni la nchi nzima kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wote wa Simba kutoka kwenye matawi, vituo mbalimbali hata kwenye makundi ya WhatsApp watafanya zoezi hilo

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER