Tutacheza mechi ya pili ya kirafiki leo

Kikosi chetu leo kinatarajia kucheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya Timu ya Abo Hamad inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri.

Mchezo huo ambao ni sehemu ya mazoezi utapigwa saa moja usiku kwa saa za hapa Misri ambapo kwa saa za nyumbani ni saa mbili usiku.

Kocha Mkuu Zoran Maki, amesema mchezo huu ni muhimu kwa ajili ya kuangalia utimamu wa mwili wa wachezaji na jinsi wanavyopokea mafunzo yake.

Kocha Maki amesema mchezo wa kwanza dhidi ya Ismailia vijana wake walicheza vizuri dakika 25 za mwanzo kwa kuwa walikuwa na nguvu lakini baada ya kuchoka wakaanza kupoteza umakini.

“Dakika za mwanzo hakukuwa na tofauti kati ya Ismailia na Simba lakini dakika za mwisho tofauti kubwa ilionekana hasa baada ya wachezaji wangu kuchoka. Tunahitaji kuendelea kupata mechi hizi ili kuwaweka sawa.

“Mechi ya leo itakuwa ni maalum kwa ajili ya kuangalia ni kwa namna gani utimamu wa mwili umeimarika na pia kuangalia ubora wa wachezaji wapya ambao hawakucheza mechi ya kwanza,” amesema Kocha Zoran.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER