Tupo ugenini Marakkech Leo

Kikosi chetu leo saa nne usiku kitashuka katika Uwanja wa Marrakech kuikabili Wydad Casablanca katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tunaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya bila kufungana ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy kutoka Botswana katika mechi iliyopita.

Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia wapinzani wetu hawajapata pointi yoyote mpaka sasa lakini tumejipanga kuhakikisha tunapambana nakupata ushindi.

Benchika atoa kauli kuhusu mchezo wa leo.. …….

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amesema haiwezi kuwa mechi nyepesi, Wydad ni miongoni mwa timu bora Afrika bila kujalisha matokeo waliyopata kwenye mechi zao zilizopita.

Kuhusu maandalizi ya mchezo Benchikha amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na wamefika Morocco mapema hivyo wamezoea hali ya hewa ingawa haina tofauti kubwa na jijini Dar es Salaam.

Ngoma nae azungumzia mchezo……..

Kiungo mkabaji Fabrice Ngoma amesema pamoja na ugumu ambao tunatarajia kuupata kutoka kwa Wydad lakini tupo kamili kuwakabili.

Ngoma amesema kwenye hatua hii hakuna mechi nyepesi kila timu imejiandaa lakini tupo kamili kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

“Tunaiheshimu Wydad ni timu bora Afrika, ina kikosi imara lakini nasi tumejipanga na tupo tayari,” amesema Ngoma.

Walitufunga mara ya mwisho tulivuokutana.

Aprili 28 mwaka huu tulikutana na Wydad katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa katika Uwanja wa Mohamed V na kupoteza kwa bao moja.

Mchezo ulienda kwenye hatua ya penati tukatolewa kwakuwa Aprili 22 tuliwafunga bao moja Uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.

Mechi ya pili ya kocha Benchikha.

Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha leo ataiongoza timu kwa mara ya pili baada ya sare ya bila kufungana tuliopata ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy, Disemba Mosi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER