Tupo tayari kwa Derby ya Dar

Kikosi chetu kiko tayari kuelekea mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni.

Mchezo huu huvuta hisia za wadau wengi wa soka ndani na nje ya nchi ni wa kwanza kwa msimu huu mpya wa 2021/22 ambapo tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Wachezaji wote wamefanya mazoezi ya mwisho jana jioni na kila mmoja amejaribu kulishawishi benchi la ufundi ili kupata nafasi ya kuanza.

PABLO AKIRI ITAKUWA MECHI NGUMU

Akizungumzia mchezo huo,bKocha Mkuu Pablo Franco, amesema utakuwa mgumu na Derby siku zote inakuwa hivyo lakini tumejiandaa kupata alama tatu ili kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Itakuwa mechi ngumu lazima tukubali hilo lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu na kupata alama tatu muhimu,” amesema Pablo.

BARBARA AWAITA MASHABIKI KWA MKAPA

Naye Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez, amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwapa ‘sapoti’ wachezaji ili tupate ushindi mnono.

Barbara amesema tunahitaji kupata ushindi katika mchezo wa leo ambao utatufanya kukaa katika msimamo wa ligi na pia tunahitaji kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Kikubwa mashabiki wetu tunawaomba mjitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu tunahitaji pointi tatu muhimu, kila kitu kinaenda sawa,” amesema Barbara.

NI MECHI YA KUTAFUTA MBABE

Kwa mujibu rekodi ya michezo nane ya mwisho tuliyokutana kila timu imeshinda mechi mbili na sare nne hivyo leo tunatafuta mbabe.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER