Tupo tayari kumalizia Kazi tuliyoanza kwa Mkapa

Kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Cairo International leo saa 11 jioni kuikabili Al Ahly katika mchezo wa marudiano wa African Football League

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 20 tulitoka sare ya mabao 2-2.

Tunahitaji kushinda mchezo huu ili kutinga nusu fainali ya michuano hii ingawa tunajua haitakuwa kazi rahisi kutokana na ubora wa Al Ahly hasa wakiwa kwao.

Robertinho kuja na mbinu tofauti…..

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa atakuja tofauti kulinganisha na tulivyocheza mchezo kwanza jijini Dar es Salaam juzi.

Robertinho amesema anategemea pia kufanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji ambao wataendana na mpango wa mechi ya leo.

“Mchezo uliopita tulicheza vizuri zaidi kipindi cha pili, nataka tuanze hivyo leo lakini tutakuwa tofauti kidogo kuanzia kwenye upangaji wa timu.”

“Pamoja nakuwa tunaiheshimu Al Ahly lakini tumekuja Misri kwa lengo la kupambana tushinde mchezo na tufuzu nusu fainali,” amesema Robertinho.

Wachezaji hawajakata tamaa…..

Pamoja na kutoka sare ya mabao 2-2 nyumbani wachezaji hawajakata tamaa na wanaamini wanaweza kufanya maajabu ugenini.

Kiungo mshambuliaji, Willy Essomba Onana amesema dakika 90 za leo tutazipambani kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

“Kwenye mpira hakuna kisichowezekana, hata sisi tunaweza kupata mabao mawili kwao, kikubwa wachezaji tupo tayari kupambana,” amesema Onana.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER