Tupo tayari kuikabili Tabora Kesho

Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema kikosi chetu kipo kwenye hali nzuri kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tabora United utakaopigwa katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi saa 10 jioni.

Fadlu amesema amekiandaa kikosi kuelekea mechi zote 15 za mzunguko wa pili huku akiweka wazi kuwa zitakuwa ngumu kutokana na kila timu kujipanga vizuri.

Fadlu amesema mchezo wa kesho dhidi ya Tabora utakuwa tofauti na ule tuliocheza mzunguko wa kwanza kwakuwa wapinzani wamejipanga vizuri na hawatapenda kupoteza tena wakiwa nyumbani lakini tupo tayari kuwakabili.

“Tumejipanga kwa ajili ya mechi zote za mzunguko wa pili tukianza kesho dhidi ya Tabora. Tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejipanga kucheza aina ya soka letu ingawa itategemea na hali ya Uwanja utakavyokuwa,” amesema Fadlu.

Akizungumzia hali ya kikosi Fadlu amesema “kiungo mshambuliaji Awesu Awesu ambaye alipata maumivu kwenye mechi dhidi ya Kilimanjaro Wonders hatakuwa sehemu ya mchezo pamoja na mlinda mlango Aishi Manula anayesumbulia na mafua lakini wengine wote wapo tayari.”

Kwa upande wake mlinda mlango, Ally Salim amesema kwa upande wa wachezaji wapo tayari kufuata maelekezo watayopewa na walimu na kila mchezo ni fainali.

“Sisi tutaingia uwanjani kucheza kwa kufuata maelekezo ya walimu wetu, kuhusu ahadi walizoaahidiwa wapinzani wetu hazituumizi kichwa na wala hazitatutoa mchezoni badala yake tutafuata mbinu zetu,” amesema Salim.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER