Tupo tayari kuikabili KMC

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi kuikabili KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tunaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu nzuri ya mabao 3-0 tuliopata katika mechi ya ligi dhidi Kagera Sugar.

Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa KMC, tutaingia kwa kuwaheshimu lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

Hiki ndicho alichosema Kocha Matola……

Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema kikosi kipo vizuri na kimepata maandalizi kuelekea mchezo ambao tutaingia kwa lengo na kuhakikisha tunapata pointi tatu.

Matola amesema wachezaji na benchi la ufundi wamejipanga kiufundi na kisaikolojia kwa ajili ya kuwakabili KMC.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo, tunajua itakuwa mechi ngumu na mara zote KMC inatupa upinzani mkubwa lakini tupo tayari kuhakikisha tunashinda.

“Wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja baada ya mchezo dhidi ya Wydad Casablanca na baada ya hapo wameendelea na mazoezi na hadi jana na sasa wapo tayari kwa mchezo,” amesema Matola.

Duchu atoa ya moyoni……

Akizungumzia kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia David Kameta ‘Duchu’ amesema pamoja na ugumu ambao tutakutana nao mbele ya KMC lakini tupo tayari kwa mchezo.

“Tupo tayari kwa mchezo na lengo letu ni kuhakikisha tunapambana hadi mwisho ili kupata pointi tatu,” amesema Duchu.

Chama, Kapama kuikosa KMC…….

Viungo, Clatous Chama na Nassor Kapama hawatakuwa sehemu ya mchezo wa leo baada ya kufungiwa na Uongozi kutokana na utovu wa nidhamu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER