Tupo Tayari kuikabili Dodoma Jiji

Leo saa 12:30 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Jamhuri kuikabili Dodoma Jiji katika muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tutaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 tuliopata katika mechi iliyopita dhidi ya Azam FC.

Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Dodoma kutokana na ubora walionao lakini tumejiandaa kuwakabili.

Hichi ndicho Alichosema Kocha Fadlu……

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika na tupo tayari, ratiba ni ngumu lakini tupo tayari na malengo yetu ni ushindi.”

“Kikosi kipo kwenye umbo zuri najivunia timu yangu kwa jinsi tunavyocheza,” amesema Kocha Fadlu.

Kijili atoa neno…..

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia, Kelvin Kijili amesema kwa upande wao wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ingawa amekiri utakuwa mgumu.

“Tupo tayari kwa mchezo, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejiandaa na lengo likiwa ni kuchukua pointi zote tatu,” amesema Kijili.

Mara ya mwisho tuliwafunga Jamhuri…..

Katika mchezo wa mzunguko wa pili msimu uliopita kwenye Uwanja wa Jamhuri tulipata ushindi wa bao moja.

Bao hilo lilifungwa na Freddy Michael Kouablan dakika ya saba baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Edwin Balua.

Manula, Chasambi waongezwa…..

Mlinda mlango Aishi Manula na winga Ladaki Chasambi ambao hawajacheza mechi zilizopita wamejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 22 kilichokwenda jijini Dodoma.

Kagoma, Mzamiru bado….

Viungo wetu wakabaji Yusuph Kagoma na Mzamiru Yassin bado wataendelea kuwa nje na hawakusafiri na timu kuja Dodoma kwakuwa wanaendelea na matibabu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER