Tupo Sokoine Leo kuikabili Prisons

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wetu wa nne wa Ligi Kuu ya NBC.

Mchezo wa leo utakuwa wa kwanza wa ugenini msimu huu baada ya mechi zetu tatu za kwanza tukicheza tukiwa nyumbani.

Haijawahi kuwa mechi rahisi mara zote tunapokutana na Prisons hasa katika Uwanja wa Sokoine hivyo tutaingia kwa tahadhari kubwa kwakuwa lengo letu ni kuchukua alama tatu.

KIKOSI KIPO TAYARI

Kocha wa muda, Juma Mgunda amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na tunafahamu utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani hasa wanapokuwa nyumbani.

Mgunda amesema timu imepata siku mbili ya kufanya mazoezi baada ya kurejea kutoka Malawi tulipokuwa na mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets.

“Kikosi kipo kwenye hali nzuri, tumepata siku mbili za kufanya mazoezi jana na leo, tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari kupambana kuhakikisha tunarudi na pointi zote tatu,” amesema Mgunda.

KANOUTE, AKPAN KUUKOSA MCHEZO

Viungo wetu wawili wakabaji Sadio Kanoute na Victor Akpan hawatakuwa sehemu ya mchezo wa leo kutokana na sababu tofauti.

Akpan anaendelea kuuguza majeraha wakati Kanoute anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano hivyo kanuni haziruhusu kuwa sehemu ya mchezo wa leo.

TULIPOTEZA MECHI YA MWISHO SOKOINE

Mara ya mwisho tulivyokutana na Prisons katika Uwanja wa Sokoine, Juni 26 mwaka huu tulipoteza kwa kufungwa bao moja.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER