Tupo Obeid Ituni Chilume Leo

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Obeid Ituni Chilume kuibali Jwaneng Galaxy katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tunaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya kufungana bao moja tukiwa nyumbani dhidi ya ASEC Mimosas kutoka Ivory Coast.

Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu hasa kwakuwa tupo ugenini lakini tumejipanga kuhakikisha tunapambana tunapata ushindi.

Mchezo wa kwanza wa Benchika…..

Mechi ya leo ni ya kwanza ambayo kocha Abdelhak Benchikha atakiongoza kikosi chetu tangu alipopewa kibarua hicho mapema wiki hii.

Benchikha ameongeza mazoezi ya timu kwa siku tatu yakiwepo ya jana ya mwisho tuliyofanya katika Uwanja wa Obeid Ituni Chilume.

Benchikha yeye anataka mataji tu……..

Katika mazungumzo yake mara zote anawasisitiza wachezaji kuwa anataka mataji ambapo ndoto hiyo itakuwa ngumu kutimia kama wachezaji hawatafuata maelezeko yake.

Benchikha amewaambia wachezaji kuwa anawaamini na yupo tayari kufanya kazi na kila mmoja kinachotakiwa kila mtu atimize majukumu yake anayopewa.

Zimbwe Jr afunguka…….

Nahodha Msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa wapo tayari kujitoa kwa dakika zote 90 kuhakikisha timu inapata ushindi.

“Sisi wachezaji tupo tayari, kila mmoja morali yake ipo juu na akipewa nafasi atakuwa kamili kwa ajili ya kuipigania timu kupata ushindi,” amesema Zimbwe Jr.

Tuliwapiga 2-0 Obeid Ituni Chilume…….

Mchezo wa mwisho tulipokutana na Galaxy katika Uwanja wa Obeid Ituni Chilume, Oktoba 17, 2021 tuliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mabao hayo yalifungwa na kiungo Taddeo Lwanga dakika ya tatu na nahodha John Bocco dakika ya sita.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER