Tupo Meja Jenerali Isamuhyo kuikabili JKT Leo

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tutaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu nzuri ya kupata ushindi kwenye mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Geita Gold uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo ulio mbele yetu kwakuwa tunahitaji kutwaa ubingwa wa Ligi msimu huu.

Mkakati wa Benchi la Ufundi……..

Kocha wa Makipa, Daniel Cadena amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri.

Cadena amesema licha ya ratiba kuwa ngumu kutokana na kucheza mechi kila baada ya siku mbili tumejipanga vizuri kuhakikisha tunawapa furaha mashabiki kwa kupata pointi tatu.

“Tunajivunia kuwa na wachezaji bora ambao wanacheza kila baada ya siku mbili lakini wanapambana na kuhakikisha tunapata ushindi.” amesema Cadena.

Wachezaji wapo tayari kwa mchezo…….

Nahodha wa timu, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wachezaji wanajua utakuwa mchezo mgumu lakini wamejipanga kuhakikisha tunashinda.

“Haitakuwa mechi rahisi, tunawajua JKT ni timu nzuri lakini tumejipanga na tutaingia kwenye mchezo wa kesho kwa lengo la kutafuta pointi tatu,” amesema Zimbwe Jr.

Ni mara ya kwanza kucheza Meja Jenerali Isamuhyo……

Itakuwa mchezo wa wetu wa kwanza kucheza Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo kwahiyo matokeo yoyote yatayo tokea itakuwa ni historia kwetu.

Onana nje wiki moja…………

Katika mchezo wa leo tutaendelea kumkosa kiungo mshambuliaji Willy Onana kutokana na kuuguza jeraha lake ambapo atakuwa nje kwa wiki moja zaidi ili kupona kabisa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER