Tupo Liti kuikabili Ihefu Leo

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Liti mkoani Singida kuikabili Ihefu FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tunaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa tunafahamu tunaenda kukutana na timu bora yenye wachezaji wazuri wenye uzoefu.

Tunahitaji kupata pointi tatu kwenye mchezo wa leo kila mechi kwetu ni fainali.

Matola: Njoo Liti tutawalipa furaha…..

Kocha Msaidizi Seleman Matola amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa leo kwa ajili ya kuisapoti timu nasi tutawalipa furaha.

Matola amesema anajua mashabiki hawana furaha hasa baada ya timu kutolewa kwenye mashindano mawili mfululizo lakini leo ndio siku ya kuwarejeshea furaha yao.

“Tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kesho, tunajua wameumizwa na matokeo yetu ya mechi zetu zilizopita lakini tumejipanga, tunawaahidi tutawapa furaha,” amesema Matola.

Wachezaji wanaitaka mechi……….

Nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wachezaji wapo tayari kupambana na kila mmoja yupo kamili.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo wa kesho, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejiandaa vya kutosha,” amesema Zimbwe Jr.

Inonga yupo fiti kuikabili Ihefu…..

Mlinzi wa Henock Inonga yupo fiti kwa ajili ya mchezo wa leo na jana amefanya mazoezi ya mwisho kikamilifu pamoja na wenzake na Kocha Abdelhak Benchikha akiona inafaa atamchezesha.

Inonga alipata maumivu katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly wiki iliyopita na kupelekea kuukosa mchezo wa dhidi ya Mashujaa FC lakini sasa yupo tayari kwa ajili ya mechi ya leo.

Tuliwafunga kwa Mkapa…..

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 28 mwaka jana tuliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Katika mchezo huo mabao yetu yalifungwa na Jean Baleke na Moses Phiri.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER