Tupo kwa Mkapa Leo kuikabili Kagera

Kikosi chetu leo kitashuka katika dimba la Benjamin Mkapa saa moja usiku kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambao tunataraji utakuwa wa upinzani mkubwa.

Tunaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi mnono wa mabao 4-1 tuliopata wikiendi iliyopita dhidi ya Ruvu Shooting.

Lakini pia tutaingia katika mchezo wa leo kwa tahadhari kubwa kwa kuwa tunajua Kagera ni timu nzuri pia tunakumbuka tulipoteza mbele yao katika mechi ya mzunguko wa kwanza.

PABLO ATOA NENO

Kocha Mkuu Pablo Franco amesema mchezo utakuwa mgumu na upinzani mkubwa kutokana na ubora wa timu zote lakini itakayokuwa bora zaidi uwanjani itaibuka na ushindi.

“Mchezo utakuwa mgumu, Kagera ni timu nzuri na tunakumbuka walitufunga katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ingawa nasi tulipoteza nafasi nyingi za kufunga.

“Tunahitaji kuwapa furaha mashabiki wetu ambao mara zote wamekuwa nasi katika nyakati za furaha na huzuni. Tutawakosa baadhi ya wachezaji wetu muhimu kutokana na kuwa majeruhi lakini waliopo wapo tayari kupambana,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER