Tupo kamili kwa Mzizima Derby leo

Kikosi chetu leo kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ‘Mzizima Derby’ utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja jioni.

Tunajua mchezo utakuwa mgumu kwani hii Derby inashika nafasi ya pili kwa ukubwa nchini, Azam wana timu nzuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Mara zote tunapokutana na Azam mechi haijawahi kuwa nyepesi tunategemea kupata upinzani mkubwa na tunaamini mchezo utakuwa wa kuvutia.

ALICHOSEMA KOCHA MGUNDA

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wako kwenye hali nzuri tayari kupigania timu kupata alama tatu.

Mgunda amesema mchezo utakuwa mgumu kwa sababu unakutanisha timu bora na tumechukua tahadhari zote kwa kuwa lengo letu ni kuhakikisha tunashinda.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, tunajua itakuwa mechi ngumu, tunaiheshimu Azam ni timu bora lakini tupo tayari kupambania alama tatu,” amesema Mgunda.

GADIEL ATOA NENO

Mlinzi wa kushoto Gadiel Michael amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kutupa sapoti kama wanavyofanya mara zote ili malengo ya kupata alama tatu yafanikiwe.

“Mashabiki ni watu muhimu na wana mchango mkubwa kufanikisha timu kupata alama tatu, mara zote wamekuwa msaada na tunajua Wanasimba watakuja sababu hawajawahi kutuacha,” amesema Gadiel.

WANNE KUIIKOSA DERBY

Katika mchezo wa leo tutakosa huduma ya wachezaji wanne kutokana na sababu tofauti.

Wachezaji hao ni Sadio Kanoute, ambaye anaugua tonsils (mafindofindo) ambapo anaendelea vizuri na ameanza mazoezi ya gym, Israel Patrick, amepata majeraha katika mchezo uliopita dhidi ya Yanga, huenda akawa nje ya uwanja kwa wiki mbili.

Wengune ni Jimmyson Mwanuke ambye bado anendelea kuuguza majeraha na Mzamiru Yassin anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER