Tupo kamili kuwavaa Mbeya City leo

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Sokoine kuikabili Mbeya City mtanange wa Ligi Kuu ya NBC ambao tunatarajia utakuwa mgumu lakini wa kuvutia.

Wachezaji wote wamefanya mazoezi ya mwisho jana jioni na hakuna yoyote ambaye tutamkosa kutokana na majeruhi au adhabu ya kadi.

Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja amejitahidi kufanya vizuri mazoezini ili apate nafasi ya kucheza.

HII NDIYO KAULI YA KOCHA PABLO

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na uwezo wa wapinzani ukichangiwa pia na aina ya uwanja ambao tutatumia.

“Mchezo utakuwa mgumu, Mbeya City ni timu bora, tunaenda kucheza kwenye uwanja ambao hauta turuhusu kucheza mpira wa chini. Tunahitaji kuwa makini na mipira ya kutengwa ili tuwe salama,” amesema Pablo.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji, Shomari Kapombe amesema tunahitaji kushinda ili kuendelea tulipoishia baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi Alhamisi iliyopita.

“Tumetoka kushinda Mapinduzi, tunapaswa kushinda tena leo ili kuendeleza morali ya kufanya vizuri kwenye ligi ambayo tumerejea,” amesema Kapombe.

‘HEAD TO HEAD’

Katika mechi tano zilizopita tulizokutana na Mbeya City tumeshinda zote hivyo tuna nafasi ya kufanya vizuri ingawa haitupi uhakika wa asilimia 100.

22/06/2021 Simba 4-1 Mbeya City

13/12/2020 Mbeya City 0-1 Simba

24/06/2020 Mbeya City 0-2 Simba

03/11/ 2019 Simba 4-0 Mbeya City

03/05/ 2019 Mbeya City 1-2 Simba

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER