Tupo Kamili kuwakabili KMC Kirumba leo

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa CCM Kirumba kuikabili KMC katika muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Maandalizi ya mchezo yamekamilika ambapo kikosi kiliwasili juzi kutoka Kagera tulipocheza na Kagera Sugar na leo tumefanikiwa kufanya mazoezi siku tatu hapa jijini Mwanza kabla ya mechi ya leo.

Tutaingia kwenye mchezo kwa kuiheshimu KMC kwani tunajua ni timu nzuri tumechukua tahadhari zote kwa lengo la kuhakikisha tunapata pointi zote tatu.

KOCHA MGUNDA AFUNGUKA

Mgunda amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kushuka katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Mgunda ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu na tunaiheshimu KMC, tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunashinda na kuchukua alama zote tatu.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, kikosi kipo tayari kuwakabili KMC, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Mgunda.

SAIDO ATIA NENO

Nyota mpya Saido Ntibazonkiza amesema ligi ya msimu huu ni ngumu na kila timu imejipanga vizuri lakini ubora wa kikosi tulio nao anaamini tutafanya vizuri na kuchukua ubingwa.

Akizungumzia mchezo wa leo Saido amesema utakuwa mgumu na KMC ni timu nzuri lakini Simba ni bora zaidi yake na anaamini tutapata alama zote tatu.

“Mchezo utakuwa mgumu, KMC ni timu bora ina wachezaji wazuri lakini Simba ni bora zaidi na tunaamini tutaweza kupata alama zote tatu,” amesema Saido.

PHIRI KUIKOSA KMC

Mshambuliaji kinara Moses Phiri ndiye mchezaji pekee ambaye atakosekana kwenye mchezo wa leo kutokana na kupata majeraha katika mechi iliyopita lakini wengine wote wapo tayari.

TULITOKA SARE YA 2-2 KWA MKAPA

Mchezo wetu wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Septemba 7 ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Mabao yetu yalifungwa na washambuliaji Moses Phiri pamoja na Habib Kyombo katika kila kipindi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER