Tupo Kamili Kuivaa Namungo Leo

Kikosi leo saa 12:30 jioni kitashuka katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi kuikabili Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Mechi za mzunguko wa pili ni ngumu na timu nyingi huwa zimekuwa zikijiandaa vema lakini tumejiandaa kuhakikisha tunafanya vizuri katika kila mchezo.

Tunategemea utakuwa mchezo mgumu na tutaingia uwanjani kwa kuwaheshimu Namungo lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu ugenini.

Fadlu afurahishwa na maandalizi

Kocha Mkuu, Fadlu Davids amesema timu imepata maandalizi ya kutosha hasa baada ya mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji kuahirishwa.

Fadlu amesema anategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Namungo hasa ukichangiwa na uzoefu wa wa kocha Juma Mgunda.

Fadlu ameongeza kuwa lengo la kwanza kwenye mchezo wa leo ni kupata pointi tatu na la pili ni kuhakikisha tunapata mabao mengi ambayo yatatawanyika kila eneo bila kutegemea mchezaji mmoja.

“Mpango wetu ni kuhakikisha magoli yanapatikana pande zote ndio maana unaona walinzi Shomari Kapombe na Mohamed Hussein wanahusika kwenye kufunga na kutoa ‘asisti’ viungo na washambuliaji ni jukumu lao pia lakini hatutaki kuwapa presha washambuliaji wetu,” amesema Fadlu.

Duchu azungumzia ugumu wa mchezo

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia, David Kameta ‘Duchu’ amesema tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Namungo lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kupata pointi tatu ugenini.

Duchu ameongeza kuwa tumekuwa tukipata wakati mgumu tunapokutana na Namungo katika uwanja wa Majaliwa lakini tupo tayari kupambana hadi mwisho ili kufanikisha malengo.

“Mchezo dhidi ya Namungo haujawahi kuwa rahisi, katika miaka miwili iliyopita hatujapata ushindi hapa lakini tumekuja kamili kuhakikisha tunashinda,” amesema Duchu.

Hatujapata ushindi Majaliwa misimu miwili

Katika misimu miwili iliyopita hatujapata ushindi dhidi ya Namungo katika Uwanja wa Majaliwa kitu ambacho tunataka kuvunja mwiko.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER