Tupo CCM Kirumba kuikabili Geita Gold

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuikabili Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tutaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya kupata sare ya kufungana bao moja dhidi ya Azam FC ambao ulifanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba siku ya Ijumaa.

Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu lakini lengo letu ni kupambana kupata pointi tatu muhimu.

Benchi la Ufundi latoa mikakati ya mechi…..

Kocha wa Makipa, Daniel Cadena amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri.

Cadena amesema pamoja na ugumu wa ratiba kuwa ngumu tunacheza kila baada ya siku mbili lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Cadena amesema malengo ni kushinda kila mchezo uliopo mbele yetu kwakuwa tunahitaji kutwaa ubingwa wa Ligi msimu huu.

“Tupo tayari kwa mchezo wa leo, haitakuwa mechi rahisi kutokana na ubora wa wapinzani na jambo jema ni kwamba hatuna mchezaji majeruhi,” amesema Cadena.

Kazi: Kwetu kila mchezo ni fainali………

Mlinzi wa kati Hussein Kazi amesema malengo yetu ni kuchukua taji hivyo tunahitaji kushinda kila mchezo ni kama fainali.

Kazi amesema Geita ni timu nzuri na haijawahi kuwa mechi nyepesi kucheza dhidi yao lakini kila mchezaji anajua umuhimu wa kupambana hadi mwisho kufanikisha malengo.

“Ligi ni ngumu, kwetu kila mchezo ni fainali. Bado tupo kwenye kupigania ubingwa mechi bado ziko nyingi na tunaanza kesho dhidi ya Geita,” amesema Kazi.

Hali ya kikosi…………

Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na hakuna yoyote ambaye amepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa leo.

Wachezaji hao jana jioni wamefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa CCM Kirumba na wapo tayari kwa mchezo wa leo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER