Tupo CCM Kirumba kuikabili Azam Leo

Leo saa 10 jioni tunashuka katika Uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tutaingia katika mchezo huu tukiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi mnono wa mabao 4-0 tuliopata ugenini dhidi ya Tabora United.

Pia tutaingia katika mchezo wa leo tukiwa tunajua utakuwa mgumu kutokana na ubora walionao na pia kwakuwa ni Derby hivyo tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi.

Alichosema Kocha Matola kuelekea mchezo wa leo…….

Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema kikosi chetu kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo tupo tayari kupambana na lengo likiwa kupata pointi tatu.

Matola ameongeza kuwa utakuwa mchezo mgumu kwakuwa ni ‘Derby’ na unahusisha timu ambazo zinapigania ubingwa lakini hata hivyo tumejipanga kuwakabili.

“Mara zote tunapokutana na Azam haiwezi kuwa mechi nyepesi, Azam ni timu kubwa na ina kikosi bora kwahiyo tunategemea kupata upinzani mkubwa ingawa tumejipanga kushinda,” amesema Matola.

Zimbwe Jr aongea kwa niaba ya wachezaji……

Nahodha msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ Jr’ amesema wao kama wachezaji wapo kamili na kila atayepata nafasi ya kucheza atakuwa tayari kuipigania timu.

“Morali za wachezaji zipo juu, tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Azam lakini tupo tayari kupambana na mwisho wa siku tupate pointi tatu,” amesema Zimbwe Jr.

Hali ya Kikosi…….

Kocha Matola amesema wachezaji wote tuliosafiri nao wapo kwenye hali nzuri na wameshiriki mazoezi ya mwisho jana jioni na hakuna yoyote aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa leo.

Ni kama mechi ya fainali…..

Ukiacha ugumu wake kutokana na kuhusisha timu mbili bora lakini ni kama fainali kutokana na msimamo wa Ligi ulivyo mpaka sasa.

tupo nafasi ya tatu tukiwa na pointi 29 na Azam wapo nafasi ya pili na alama zao 31 hivyo kama tutashinda leo tutawashusha na kukaa juu yao

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER