Tupo Ali Hassan Mwinyi kuikabili Tabora Leo

Leo saa 10 jioni tunashuka katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kuikabili Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tutaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao moja ugenini tuliopata Jumamosi iliyopita dhidi ya Mashujaa FC.

Matola: Haitakuwa mechi rahisi

Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema mchezo utakuwa mgumu na tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Tabora lakini tumejiandaa kuhakisha tunashinda.

Matola amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na wameshiriki mazoezi ya mwisho na hakuna yoyote aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo

“Tumefika salama mkoani Tabora, wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Tabora lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Matola.

Ngoma ajiunga na kikosi……..

Kiungo mkabaji Fabrice Ngoma amejiunga na timu jana na kama benchi la ufundi litaona inafaa litamtumia kwenye mchezo wa leo.

Ngoma aliukosa mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa kutokana na masuala binafsi na alichelewa kurejea nchini lakini sasa yupo pamoja na timu.

Ni mechi ya kwanza kukutana na Tabora….

Mchezo wa leo ni wa kwanza kukutana na Tabora United kwenye Ligi kwakuwa ndio wamepanda msimu huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER