Tunazitaka pointi tatu za Ruvu Shooting

Kikosi leo chetu kitashuka katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuikabili Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambao tunategemea utakuwa mgumu na wa kuvutia.

Katika mchezo wa leo tunahitaji alama tatu ili kuendelea kuwasogelea wanaoongoza na hatimaye turudi kwenye nafasi yetu tuliyoizoea.

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema wachezaji wote wapo tayari na wameendelea kufanya vizuri kwenye mazoezi ili kulishawishi benchi la ufundi kuwapa nafasi katika mchezo wa leo.

Pablo amesema wachezaji wote 24 waliosafiri kuja jijini Mwanza wapo fiti na wamefanya mazoezi ya mwisho jana katika Uwanja wa Kirumba tayari kwa mchezo wa leo.

“Tupo tayari kwa mchezo, wachezaji wapo kamili na tumajipanga kuhakikisha tunashinda. Ruvu ni timu nzuri inacheza kitimu tunaamini watatupa ushindani lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda.

“Tutawakosa baadhi ya wachezaji kutokana na sababu tofauti lakini Simba ni timu kubwa ina wachezaji wengi bora ambao wanaweza kutumika kwenye mchezo wowote,” amesema Pablo.

TAKWIMU ZETU ZA MECHI TANO ZILIZOPITA

Idadi ya mechi 5

Mechi tulizoshinda 3

Tulizotoka sare 2

Hatujapoteza mchezo wowote

Magoli ya kufunga 3

Hatujafungwa bao lolote.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER