Tunazihitaji alama tatu pekee leo Kaitaba

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Kaitaba kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambao tunahitaji ushindi ili kurejesha hali ya kujiamini.

Baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi mbili zilizopita leo tutahakikisha tunapambana kwa dakika zote 90 ili kuibuka na alama zote tatu.

Wachezaji wote waliosafiri kwenda Kagera wapo kwenye hali nzuri na wamefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Kaitaba jana jioni tayari kwa mchezo wa leo.

KOCHA PABLO

Kocha MkuuPablo Franco, amesema mchezo utakuwa mzuri kutokana na uimara wa wapinzani pamoja na ubora wa uwanja ambao unaruhusu kuchezwa soka la aina yoyote.

Pablo amesema Kagera ni timu nzuri na ipo kwenye kiwango bora kwa sasa lakini tumejipanga kushinda ili kurejesha hali ya kujiamini kwa wachezaji pamoja na mashabiki.

“Mchezo utakuwa mzuri hata kuutazama sababu sehemu ya kuchezea ni nzuri kwa hiyo kila timu itakuwa na uwezo wa kucheza tofauti na mechi zetu zilizopita.

“Tunajua mechi itakuwa ngumu, Kagera ni timu nzuri inacheza soka safi na wapo kwenye kiwango bora sasa lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER